Familia katika Huduma – eBook

8,95 

Category:

Description

Maisha marefu, ushirika wenye furaha na familia imara – ni nani asiyetaka? Ndoto hii inayoishi katika kila mmoja wetu inaweza kuwa bayana lakini haitokei kama ajali. Yale yenye manufaa yanahitaji kupandwa, kufunzwa, kushughulikiwa na kulindwa. Mpango wa Mungu ni kwamba familia iwe salama na mazingira bora ambayo watoto watakuzwa na kuendelea katika njia sawa, wakijifunza tabia ambayo watajenga maisha yao ya baadaye.

Familia ndio kiungo kidogo zaidi katika jamii, kwa hivyo familia imara huzalisha jumuiya zilizo na afya. Kama ‘Familia katika huduma’, sisi ni sehemu ya jumuiya na tuna fursa na wajibu kuishi maisha yetu ya ndoa na kukuza watoto wetu katika jumuiya. Lakini familia ina matatizo ulimwenguni mwote leo na cha kuhuzunisha hata familia zilizo kwenye huduma.

Tulipojiunga na YWAM miaka ishirini iliyopita tukiwa familia changa, tulikuwa na dhana ya kuwa maisha katika jumuiya ya Ukristo itatulinda na matatizo ya familia. Leo hii tunafahamu ya kuwa familia thabiti haitokei kwa ghafla. Kama Wakristo hatukwepi matatizo yanayokumba familia leo na utofauti wa maisha yetu huleta changamoto ya kipeke. Yeyote anayehusika na kueneza ufalme wa Mungu yuko
mstari wa mbele katika vita vya kiroho. Si tu kulinda vile tulivyonavyo bali inahusu kuelezea na kuwa na ushawishi wa usawa mahali tulipo.

Swali ni, kitu gani tunataka kufikia? Tutaishi namna gani kila siku ili ndoto yetu itimie? Ni vitu gani watoto wetu wanahitaji wafunzwe na ujuzi upi wanauhitaji? Mambo haya yatagharimu nini? Kanuni ya Biblia ya kupanda na kuvuna pia inahusu ndoa na familia – tunavuna tulichopanda.

Miaka mingi, tumekuwa na nafasi nyingi za kuuliza familia zingine ambazo zinahusika katika huduma kuhusu mambo ambayo wameyapitia, hasi na chanya. `Tulitafakarishwa na majibu yao pamoja na matokeo ya utafifi uliofanywa kwa muda mrefu na Dr Nick Stinnett (‘Tabia ya Familia Imara’) ambao ndio mwanzo wetu wa kuunda mafunzo ya familia katika jumuiya yetu ya YWAM Hainichen. Wahusika wote walinufaishwa kutokana na kushiriki na wengine kuhusu nafasi na changamoto walizokumbana nazo kama familia katika huduma.

Ndipo marafiki kutoka makanisa mengine na mashirika walianza kutuuliza kama tungenakili habari tulizokusanya na mambo tuliyojifunza kutoka kwa watu wetu na wengine na ujuzi waliokuwa nao. Kitabu hiki ambacho kimetolewa kimaalum kwa ajili ya ujenzi wa familia imara, ndio Matokeo yake. Kinaweza kutumiwa kama kitabu cha mafunzo, ili kuanzisha na kuhamasisha mazungumzo katika familia.

Kila sehemu katika sehemu zote nane inawakilisha ‘mahali penye shida’ ambayo tumeitambua katika miongo miwili ambayo tumeishi katika jumuiya ya Wakristo kama familia katika huduma. Pamoja na mafunzo na mwongozo wa mazungumzo kati ya waliooana, tumetoa pia mambo ya kufanya nyumbani, pia tumetoa vidokezo kwa masomo zaidi. Unapotumia nakala hii kufundishia, Mapendekezo ya majadiliano ya vikundi ni ya muhimu sana kwa masomo yako.

Kati ya sehemu na sehemu, tumeweka ushuhuda na taarifa kutoka kwa watu katika sehemu mbalimbali ulimwenguni ambao wanaishi hadi leo (au waliishi) katika familia zilizo katika huduma. Kina mama, kina baba na watu wazima hawa ambao wamekulia katika huduma, wanahusisha kwa uzoefu binafsi baraka na changamoto za kuishi kama sehemu ya familia katika huduma – mambo wanayoshukuru na mambo ambayo wangefanya kwa namna tofauti leo ikiwa wangepata nafasi kurejea kuishi sehemu fulani katika maisha yao.

Matamanio yetu ni kwamba kitabu hiki kitakusaidia kujenga familia thabiti katika huduma. Tunatumai kitakutia moyo uishi vyema kwa umoja na ufurahie maisha ya familia, pia uwe ishara ya matumaini katika dunia inayohitaji watu wa kuigwa kiungu.

Angela na Andreas Frész

Additional information

Type

Ebook (PDF)

Language

Swahili